Featured
Loading...

U-HEARD: Diamond baada ya kudaiwa kushtuka Zari alipoenda kumuona Ivan

May 22, 2017 kupitia U-heard ya XXL ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown ametusogezea story inayomuhusu mzazi-mwenza wa Zari,  Diamond Platnumz juu ya mama watoto wake huyo kwenda Hospitali kumjulia hali mume wake wa zamani Ivan.
Akizungumza kwenye kipindi hiko Diamond amesema hana namba ya Ivan lakini alishawahi kuonana naye miaka miwili iliyopita na kuhusu Zari kwenda Hospitali ni sahihi kwa sababu afya yake haikuwa nzuri na kudai kuwa amekuwa akimpigia simu ili kujua hali yake.
>>>“Sijawahi kuwa na namba ya Ivan. Nilikutana naye nilivyoenda MTV last two years. Ivan alikuwa anaumwa halafu hali yake ilikuwa serious sana kwa hiyo huwezi kushadadia kwenye mitandao. Zari ni mzazi mwenzake na ana kila haki kuhakikisha anaenda. Mimi nimekuwa mtu wa kwanza kumpigia simu kumuuliza anaendeleaje.” – Diamond
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full story..

UBUYU wa Motomoto...Huyu Ndiye Waziri wa Magufuli Anaye Banjuka na Msanii Batuli..!!!


UBUYU ulionyooka kabisa umetua kwenye meza ya gazeti hili ukidai kuwa, waziri kijana katika serikali ya Rais Dk.John Magufuli ‘JPM’, amedata kinomanoma na penzi la msanii wa filamu Bongo mwenye shepu bomba, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Ijumaa lina full stori.

Awali zilivuja taarifa kuwa, waziri huyo wa wizara nyeti ambaye ni mume wa mtu (jina lake linahifadhiwa kwa sasa) kafa, kaoza kwa mrembo huyo ambaye ni kada wa CCM na hivyo ameamua kumng’arishia maisha yake ili aweze kumfaidi vizuri.

KISIKIE CHANZO

“Kama ni kuyapatia maisha, Batuli sasa hivi kayapitia maana mheshimiwa….(anamtaja jina) ndiyo kajiweka kwake sasa hivi, anamhudumia kwa kila kitu, ndiyo maana unamuona mambo yake sasa hivi supa kuliko hata mastaa wengine,” alimwaga ubuyu mtoa habari huyo kisha akaongeza: “Kampangishia mjengo kule Kunduchi na ndinga pia kamnunulia, nyie fuatilieni mtajua ukweli wa ubuyu huu ninaowapa.”

IJUMAA KAZINI

Baada siri hiyo kuvuja, mmoja wa waandishi wetu alimpigia simu Batuli na kumuuliza juu ya madai hayo ambapo alifunguka kuwa na uhusiano na mheshimiwa huyo ila akasema, hayo si mambo ya kuandikwa gazetini kwani ni maisha yake binafsi li kujiridhisha na habari hiyo, siku nyingine mwandishi mwingine alimpigia simu na kutaka kuonana naye kwa ajili ya mahojiano maalum ambapo, siku hiyo alimtaka paparazi huyo wakutane Bahari Beach, eneo la Bakery, Kunduchi jijini Dar.

Mwandishi alipofika eneo hilo, aliona gari la kifahari, Range Rover Discovery lenye rangi nyekundu na kulifuata, ambapo Batuli alimfungulia mlango na kuondoka eneo hilo huku wakiendelea na mazungumzo.

Licha ya kuzungumza mambo mengi siku hiyo, huku mwandishi wetu wakati mwingine akimrekodi, staa huyo alimtaja mheshimiwa huyo kuonesha kuwa ndiye
anayemuweka mjini.

SIKU ILIYOFUATA

Siku iliyofuata, mwandishi wetu alipotaka kuandika habari hii alisikiliza rekodi katika maelezo ya Batuli na akaamua kumpigia simu tena ili kujiridhisha pale alipomtaja mheshimiwa huyo kuwa ndiye anayemuweka mjini ambapo hakutaka kulizungumzia tena. Hata hivyo, mwandishi wetu alimtumia ujumbe mfupi wa maandishi uliosomeka hivi; “Batuli, wakati tunazungumza kabla ya ishu nzima, ulitamka mtu uliyenaye ni (jina la waziri)…” Batuli alivyojibu “Hilo siyo geni hapo kwenu (Global) kwa msaada muulize (akimtaja mmoja wa waandishi wetu aliyewahi kuongea naye)…”

IJUMAA KWENYE MJENGO ANAOISHI BATULI

Katika kuendelea kuchimba, hivi karibuni mapaparazi wetu walifika kwenye nyumba anayoishi Batuli iliyopo Kunduchi (Uzunguni) lakini baada ya kugonga geti alitokea mlinzi na kueleza kuwa, ni kweli staa huyo anaishi hapo ila hawezi kupatikana hadi mtu anayemhitaji awe na miadi (appointment) naye.

IJUMAA LAMSAKA WAZIRI

Katika kubalansi habari hii, waandishi wetu walitumia kila njia kumpata mheshimiwa huyo lakini hakuweza kupatikana hivyo linaendelea kumsaka ikiwa ni pamoja na kuhakikisha linamnasa akiingia kwenye mjengo anaoishi Batuli kisha tutawamwagia kila kitu hapahapa.

From GlobalPublisher

Sirro: Naomba Uongozi wa Clouds Media Utoe Ushirikiano Uvamizi Siasa


Dar Es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amewataka uongozi wa Clouds Media Group kushirikiana na jeshi la polisi katika upelelezi wa tukio la uvamizi wa kituo chao cha matangazo. 
Akiongea na waandishi wa habari leo Sirro amesema kesi yoyote inahitaji ushahidi na uvamizi wa Clouds bado upelelezi wake unaendelea ukikamilika utapelekwa kwa wakili wa Serikali ili aone kama anaipeleka kesi hiyo mahakamani au kutoipeleka. "Ndugu zetu wa Clouds watoe ushirikiano kwa mpelelezi wa kesi yao, wao wanataarifa za kutusaidia kukamilika kwa upelelezi ila nasi tuweze kuipeleka katika hatua inayofuata. Na sio kwamba tukio limesahaurika bali upelezi wake unaendelea," amesema Sirro.
.
TOA MAONI YAKO HAPA

Ruge Amjibu Makonda baada ya Kudai ni Muongo

Mkurugenzi na mzalishaji wa vipindi waClouds Media Group, Ruge Mutahaba, ameijibu kauli iliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Dar Dar es salaam, Paul Makonda ya kuwa yeye ni muongo, na anafaa tu kuwa muandishi wa mashairi na nyimbo za mapenzi na ngonjera.

Ruge ametoa kauli hiyo leo katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo hicho, ambapo walikuwa na kipindi cha ‘SHUKRANI’ kwa wasikilizaji wao na watu waliowahi kuwasaidia kupata misaada.

“Kila mtu ana mtazamo wake, na huwezi kulazimisha mtazamo wa mtu ubadilike. Inasikitisha sana kuona mtu anayesambaza haya mambo ni bosi wangu, Bosi wa mkoa wetu. Yeye akipiga mhuri kitu ndio imekaa hiyo, Yeye ana nguvu zote,” amesema Ruge.

“Sasa akisema hivyo mimi ni tapeli anataka kila mtu Dar es Salaam anione hivyo. Mimi sina nguvu kwa hiyo nachagua kubaki kwenye ninacho kiamini. Tangu mwanzo nilisema mimi nataka haya mambo yaishe, cha kusikitisha huyu mtu ni kiongozi lakini anashindwa kumaliza jambo hili kwa busara na anataka kuliendeleza.

“Kuna mambo hapa yanajaribu kutengenezwa. Watu wanajaribu kutusukuma turudi kwenye mjadala ambao tulishaumaliza. Mimi ni mtu mzima , na busara inaniambia watu wazima hatuna haja ya kurudi kwenye majibizano ambayo kwangu yaliisha siku nyingi “alieleza Ruge.

Advertisement

VIDEO : RUGE AMJIBU MAKONDA BAADA YA INTERVIEW YA STAR TV


            VIDEO : RUGE AMJIBU MAKONDA BAADA YA INTERVIEW YA STAR TV  

Tatizo la Kunuka Kikwapa, Tiba Hii Hapa

Kikwapa ni tatizo la kutoa harufu mbaya sehemu ya kwapani katika mwili wa binadamu. Tatizo la kikwapa husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu chini ya kwapa.

Tatizo la Kikwapa ni kero kwa sababu husababisha mtu kutoa harufu inayokuwa kero kwako na kwa mtu mwingine aliyeko jirani yako.

Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo

-Paka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya

-Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya

-Oga kila siku na safisha nguo kwa maji safi itasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya

-Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.

-Osha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps)

-Punguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu

-Kumbuka kutumia pafyume na Spray zitasaidia kuondoa harufu mbaya kwa muda na sio kutibu tatizo moja kwa moja.

-Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili.

-Jitahidi kunyoa nywele za sehemu hii mara kwa mara.

-Epuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.

Alikiba Apewa Jina Jipya na Jay Z, Lipo Hapa

Mtandao mkubwa wa kuuza muziki wa TIDAL ambao upo chini ya rapa Jay Z umempa jina jipya msanii kutoka Bongo Alikiba na kumtambua kwa jina la 'The unstoppable' yaani mtu asiezuilika kwa kitu akifanyacho. 

"The unstoppable AliKiba is live right now in London" mtandao wa TIDAL uliandika wakati Alikiba akifanya yake kwa steji usiku huo. 

Alikiba alipewa jina hilo wakati akishiriki katika moja ya tamasha la muziki ambalo lilifanyika mwisho wa wiki nchini Uingereza ambalo lilikusanya mastaa kibao akiwepo Cassper Nyovest, P Square, Davido, Awilo Logomba, Sarkodie, Tekno , MI na wasanii wengine wengi huku bongo ikiwakilishwa na 'King' Alikiba ambaye alipata nafasi ya kufanya 'performance' ya ngoma zake kama Mwana, Unconditionally Bae na Aje.

Mashabiki wengi wameonyesha kufurahishwa na hatua hiyo ya Alikiba kushiriki katika tamasha hilo kubwa huku akiwa na wasanii wakubwa kibao, kwani wanaamini jambo hilo linazidi kumjenga na kufungua njia zaidi katika kazi yake hiyo ya muziki

Diamond Kumtambulisha Msanii Mpya wa WCB Wasafi Leo.

Rais label ya WCB, Diamond Platnumz Jumatatu hii atamtambulisha msanii mpya wa label hiyo.
Msanii huyo atakuwa msanii wa 5 kutoka ndani wa label hiyo ambayo ina wasanii 4 akiwemo Rich Mavoko, Harmonize, Rayvanny pamoja na Queen Darleen.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Marry You, amesema anafanya hivyo ili kuwasaidia wasanii wachanga ambao wanavipaji lakini wanashindwa kufikia malengo yao.
“Panapo majaaliwa siku ya Jumatatu kesho (leo), ntakuwepo kwenye Leo tena ya Clouds Fm na familia nzima ya WCB Wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu mwingine mpya toka mtaani, ndani ya WCB,” aliandika Diamond Instagram.
Aliongeza, “Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umaskini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake. Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha. Siku zote naomba mkumbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond, ni ya vijana wote wapambanaji…na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti, kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo…… USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi…Shukran”

Wolper afunguka kuachana kwake na Harmonize

Jacqueline Wolper

Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amedai aliachana na aliyekuwa mpenzi wake Harmonize miezi 3 iliyopita lakini waliamua kuficha kwaajili ya shughuli zao za kibiashara.

Muigizaji huyo ambaye alicheza vitendo kwenye video ya wimbo ‘Niambie’ wa Harmonize, amedai wakati kazi hiyo inatoka walikuwa tayari  wameachana lakini waliamua kushirikiana katika promo ya wimbo huo ambao unafanya vizuri.

“Nyie mnajua sisi tumeachana juzi? Tumeacha miezi mitatu iliyopita kabla hata ya wimbo wake Niambie haujatoka,” Wolper alikiambia kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV.

Aliongeza ,“Sisi wenyewe tuliamua kukaa kimya kwa sababu kuachana sio kugombana kuna kesho mnaweza kushirikiana katika mambo mengine ya kibiashara,”

Hata hivyo muigizaji huyo aligoma kueleza sababu ya kuachana na muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Happy Birthday’.

Halima Mdee Awachana Wabunge wa CCM

Mbunge  wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), amewatibua wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuwashangaa jinsi wanavyoisifu Serikali kutokana na kufuta tozo, kodi na ada katika sekta za uvuvi, kilimo na mifugo.

Tukio hilo lilitokea bungeni jana wakati wabunge walipokuwa wakiendelea na mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 iliyowasilishwa juzi na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Charles Tizeba.

Katika maelezo yake, Mdee aliwaambia wabunge hao kwamba pongezi zao katika kuondoa tozo hizo hazitakiwi kutolewa kwa kuwa wakulima hawajandaliwa mazingira mazuri ya kuwanufaisha na kilimo.

Kwa mujibu wa Mdee, sekta ya kilimo nchini inayohusisha asilimia 65 ya Watanzania, imekuwa ikishuka kila mwaka badala ya kupanda.

“Nashangaa sana waziri anasimama hapa na kutumia robo tatu ya hotuba yake kueleza masuala ya tozo,” alisema na kuongeza:

“Nawashangaa pia wabunge wanaosimama na kupongeza kuondolewa kwa tozo na naamini hizi pongezi zisingekuwapo kama Serikali ingekuwa imeandaa mazingira mazuri kwa wakulima hao.

“Nimesoma bajeti ya Waziri wa Viwanda, ameeleza kuna viwanda 234 vimesajiliwa kuanza, lakini viwanda vyote viko Dar es Salaam.

“Kwa tafasiri nyingine ni kwamba wabunge wa Kanda ya Ziwa ambao wanatoka katika maeneo ya kilimo cha pamba, bajeti hii haikuwaangalia kabisa ingawa mnasimama hapa na kupongeza.

“Kwa hiyo, napenda niwashauri wabunge wa CCM ambao ni wapya katika Bunge hili, kwamba kazi yetu ni kuisaidia Serikali na tunapokuwa tunatoa pongezi za aina hii wakati tukijua hali ni mbaya, tunaharibu nchi.

“Lazima wabunge wa CCM msome ilani ya chama chenu ambayo hata mimi wa chama cha upinzani huwa naisoma ili kupata maarifa na kujua jinsi mlivyojipanga.”

Pamoja na hayo, Mdee aliishutumu Serikali kwa kushindwa kutoa taarifa ya upimaji wa ardhi nchi nzima baada ya hoja yake kuungwa mkono na Bunge mwaka 2011.

Kutokana na maneno hayo, baadhi ya wabunge wa CCM walilazimika kusimama kwa nyakati tofauti na kuomba kumpa taarifa mbunge huyo.

Aliyekuwa wa kwanza kutoa taarifa ni Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi, ambaye alimkosoa kwa kusema wabunge wote ni wapya kwa kuwa walipatikana baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi.

Mwingine aliyesimama ni Mbunge wa Nyasa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya, aliyesema kuipongeza Serikali baada ya kufuta tozo hizo ni jambo la msingi kwa sababu wabunge wanajua jinsi zilivyokuwa zikiwaumiza wakulima.

Kwa upande wake, Mbunge wa Newala, George Mkuchika, alimwambia mbunge huyo kwamba kila mbunge ana uhuru wa kupongeza katika eneo analoona kuna haja ya kufanya hivyo.

Wakati hao wakisema hayo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), alisimama na kumwomba Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, amlinde Mdee kwa kuwa anachokizungumza kinatokana na vitabu vya Serikali.

Kutokana na hali hiyo, Chenge aliwataka wabunge wasiendelee kutoa taarifa kwa kuwa mwenye jukumu la kufafanua utendaji wa Serikali ni waziri mwenye dhamana.

“Kuna utaratibu mmeuanzisha hapa wa mbunge kusimama na kuomba kutoa taarifa na anayepewa taarifa hata kama ni nzuri, anaikataa.

“Lakini eleweni kwamba anayechangia hapa ni Mdee ambaye maelezo yake yanatakiwa kujibiwa na waziri mwenye dhamana,” alisema Chenge.

Juzi Dk. Tizeba wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake, alisema Serikali imefuta tozo, kodi na ada 108 zilizokuwa kero katika sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo.
© Copyright TUANGAZE BONGO
Back To Top