Irene Uwoya Asema Angeumudu ‘Ukuu’ wa Wilaya Kama Angepewa

Msanii wa filamu Irene Uwoya amefunguka kwa kusema kuwa kama angepata nafasi ya ukuu wa wilaya basi angefanya vizuri kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kuongoza.
Irene Uwoyo

Muigizaji huyo ameimbia Bongo5 kuwa hakuwa na matarajio yakuteuliwa lakini kama angeteuliwa angeitendea haki nafasi hiyo.

“Mimi sijaomba wala sijawai kusema kama nataka hiyo nafasi, lakini kama ikitokea naiweza sana, nipo vizuri sana ndio maana hata nikathutu kugombea ubunge kwa sababu nilijua naweza kuongoza,” alisema Irene Uwoya.

Muigizaji huyo mahiri aligombea ubunge wa viti maalum Tabora lakini akakosa na kuhaidi kujipanga katika uchaguzi ujao.