Juma Nature Hajaua Mtu Kwetu - Mh. Temba

Mkongwe wa Bongo Fleva amesema kwamba ambaye anaweza kuwaweka mezani yeye na Juma Nature na kuwapatanisha na wakafanya kazi yeye hana shida.

“Kwa kuwa Juma ni rafiki yangu na hakuna ugomvi wowote kati yetu kwani Juma ni rafiki yangu tangu zamani na Juma hajaua mtu kwetu” alisema Mh. Temba.
Akipiga stori na eNewz Temba amesema kwamba “Sisi kama sisi tulishawahi kulizungumza mi nikamwambia ni muhimu tuwe na watu wenye busara watuongoze katika kazi zetu kwa kuwa sisi ni wasanii wakubwa katika nchi hii isije ikatokea tukapishana kauli kidogo mambo yasiende kama tulivyokuwa tukitarajia”

Aliongeza kuwa “Hata hivyo sisi wenyewe tunaweza kujiongoza lakini akili ya muziki mi naifahamu. Nawasihi Watanzania wasubiri kazi nzuri kutoka kwetu”.