Nina Furaha Toka Nitoke CCM - Edward Lowassa


Lowassa kupitia ukurasa wake wa Facebook ameelezea furaha yake namna ambavyo ameimarika zaidi baada ya kujitoa ndani ya CCM hadi sasa ambapo ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

''Nina furaha kutimiza mwaka mmoja toka nilipojitoa CCM na kujiunga na CHADEMA.Uamuzi ule haukuwa rahisi,lakini kwa ushupavu, ujasiri na mwongozo wa Mungu nilifanya hivyo. Nilifanya uamuzi wa kihistoria katika nchi yetu'' Amesema Lowassa.

Ameongeza kuwa watanzania bado wanataka mabadiliko na hali hiyo imezidi kuthibitika kuwa wananchi hawawezi kuyapata ndani ya CCM .

Amesema watanzania wanataka sera na mtu mbadala wa kuongoza mabadiliko hayo na kwamba vyote hivyo watavipata ndani ya CHADEMA na UKAWA kwa jumla.

Aidha amewataka watanzania wanaomuunga mkono na ambao walihama CCM kwa ajili yake waendelee kumuunga mkono na kuiunga mkono CHADEMA.