Shilole alalamika kufanyiwa udhalilishaji kwenye kivuko cha Kigamboni


Msanii wa Bongo Flava, Shilole amelalamika kupitia akaunti yake ya Instagram kuwa amefanyiwa vitendo vya udhalilishaji katika kivuko cha Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Muimbaji huyo ameishia kulalamika tu na hakutaja hasa kitu gani amefanyiwa.

“Uzalendo maana yake nini??
Je kuna thamani yoyote kuwa mtanzania??
Je jitihada zozote zinazofanywa na wasanii kuitambulisha nchi yao zinathaminiwa??
Jana nimetendewa kitendo cha ajabu katika kivuko cha kigamboni na kutendewa udhalili bila kujali kuwa mimi ni mwanajamii nayegusa maisha ya watu.
Muziki ni biashara, lakini pia tuna nafasi yetu katika kuisaidia jamii na kupeleka ujumbe muhimu.
Tusiheshimiwe tunapohitajika na kudharaulika tunapohitaji tuheshimiwe.
Nimeguswa…. Nimeumia.
Someone should act. @paulmakonda @paulmakonda”

ameandika Msanii huyo