VIDEO: Edward Lowassa kaongea haya kuhusu wabunge wa upinzani kususia vikao


Vikao vya bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017 ambalo limemalizika hivi karibuni huku ikishuhudiwa wabunge wanaounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, wakitoka nje na kutohudhuria vikao hivyo.

Leo July 31 2016 kupitia kipindi cha funguka kinachorushwa na kituo cha television cha Azam Tv, Waziri mkuu wa zamani na aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa amezungumzia kuhusu wabunge wa upinzani kususia vikao vya bunge, Lowassa amesema…………..
Tutazame tatizo katika ujumla, tatizo linatokea na Spika Ndugai kuwa na hali mbaya ya afya, namfahamu Ndugai ni mtu makini sana, angekuwa madarakani mambo hayo yasingefikiwa’
Kuna tatizo pale kwanza la psychology., naibu Spika ameletwa kwa njia ambazo watu wanaona pengine hazikuwa sahihi sana na amejichukulia madaraka na anachukua maamuzi ambayo ni magumu kidogo mimi ninawaelewa wabunge wetu’ 
VIDEO: