Wolper awa kada rasmi wa CCM, mashabiki wamuita ‘Yuda Iskarioti’

Jacqueline Wolper, muigizaji aliyejipatia umaarufu mwaka jana kwa kuwa bega kwa bega na aliyekuwa mgombea urais kupitia tiketi ya Ukawa, Edward Lowassa, amejiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi, CCM.
Wolper alitangaza kujiunga na chama hicho tawala Jumamosi iliyopita kwenye mkutano mkuu uliofanyika Dodoma ambapo pia Rais Dkt John Magufuli alichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya.
Muigizaji huyo alishare kwenye Instagram picha ikimuonesha akimpa mkono Rais mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete kwenye mkutano huo.
Picha hiyo hata hivyo imesababisha hasira nyingi kwa mashabiki wake ambao ni wapenzi wa upinzani huku wakimfananisha na Yuda Iskarioti kwa madai kuwa amewasaliti Ukawa.
Hizi ni baadhi ya comments: