Zitto Utapotea, Achana na Rais Magufuli!!


Namkumbuka Zitto Zuberi Kabwe wa 2005-2010 na ninamlinganisha na huyu wa sasa mmmmhhh hadi inauma sana tukiendelea kupoteza vijana kama huyu wengine miaka ijayo kuna kazi kubwa sana ya kuja kulikomboa taifa hili!!

Nimekuwa nikijiuliza hivi Zitto ni nini kimempata??
Yuko wapi Zitto aliyeibua sakata la mgodi wa Buzwagi?
Yuko wapi zitto aliyekuwa akipigania masilai ya wanyonge bungeni kupitia ununuzi wa Rada??

Zitto aliyeungana na Dr slaa juu ya Richmond yuko wapi??
Zitto huyu huyu anayetuhumiwa kwa kuwa na mali zisizolingana na kipato chake ??
Zitto huyu huyu ambaye milija yake imezibwa pale NSSF?
Zito amekuwa mtu tena wa kupiga dili na kuakikisha kila kitu amekipata kanunua majumba mazuri ,Magari mazuri,kila kitu kamiliki leo hii kabaki na kazi moja tu ya !!

Kila siku kuiponda selikari ya Rais magufuli!!!
Hivi hakuna mazuri ya kumpongeza Rais magufuli ni kumponda tu ? Hata akipongeza anapongeza kwa unafiki!!
Kama kweli Wewe ni mzalendo unapigania masilai ya watanzania njoo ujibu maswali yafuatayo!!

Wewe si dictator??
Na ulivyo dictator ulipofika tu ACT wazalendo ukapewa cheo cha kiongozi mkuu wa chama hivi uoni kwamba ilo ni tatizo la kupenda madaraka?
Kwani kulikuwa hakuna watu wengine mpaka upewe wewe hicho cheo uligombea na nani?

Sasa hivi professor Mkumbo anawashauri wapinzani mbadilishe njia za kupambana na selikari ya Rais magufuli lakini hata ushauri usikii imekuwa sikio la kufa!
Na juzi tu mama Anna ametofautiana na wewe waziwazi kuusu mwaliko uliotolewa Dodoma !!

Mbili kwanini uliondoka chadema kwa kutaka uwe mwenyekiti uoni hapo kuna tatizo la udikiteta kutaka cheo kwa nguvu? Kwanini ukusema wazi wazi ila ukaanzisha mtandao ndani ya chama?

Ulishamsikia magufuli anagomea cheo ndani ya chama toka amejiunga na CCM hata cha mwenyekiti wa shina??
Leo hii unatoka na kumfananisha rais magufuli na Putin wa Russia hivi hoja yako ya Jana kwamba watu wamsome Putin ina faida gani kwa taifa?

Kuna faida gani kwa wananchi wa Ujiji??
Hivi unafikiri wananchi wa vijijini wanaweza kaa wasome vitabu au wapekue Internet kwa vifulushi vipi hivi hivi vya wanyonyaji Voda,Tigo na Airtel?
Baada ya kuishauri selikari ilifufue shirika letu la TCCL ili tupate affordable bundle wananchi waweze kupata Internet ilivyo bora na kuepukana na makampuni ya wanyonyaji upo tu kukosoa !!

Mkuu Zitto tulikuheshimu sana lakini sasa your politically finished!!
Baada uungane na Magufuli mpeleke kiwanda cha nyavu za kuvulia Dagaa ujiji ??unaangaika eti wananchi wamsome Putin Hivi mwananchi wa kawaida wa ujiji atakuelewa kweli??


Kwanza tu nikufaamishe taarifa nyingi unazozisoma kwenye mitandao kuusu Putin kama hazitoki Russia ni za kupika kutoka nchi za magaribi!!
Nchi za magaribi hazimpendi Putin kwa sababu analeta mabadiliko ya kweli uko Russia!!
Ni kiongozi imara asiyeteteleka kama alivyo Magufuli hivyo vyombo vya habari vya magaribi haviwezi kumpamba hata kidogo Putin ni kiongozi imara kama alivyo Magufuli!!

Ushauri kwako kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo!!
Watu unaotakiwa kubishana nao ni Mkuu wa mkoa Kigoma,Mkuu wa willaya jimboni kwako,Mkurugenzi jimboni kwako na spika wa ubunge Hao ndio size yako!! Hakuna mtu anayeupata Urais kwa kumponda Rais aliyeko madarakani hapa Afrika nikukumbushe lazima tuambiane ukweli!!

Tanzania- Professor Lipumba aliponda ameenda,
Kenya-Raila Odinga aliponda huyo anakwenda,
Uganda-Kiza Besige aliponda anakwenda,
Zimbabwe- Morgan Shangelai aliponda amekwenda !!

Mifano ipo mingi tu ila nikushauri pigania masilai ya wananchi wako wa ujiji na Tanzania!!
Nasikitika tunapoteza nguvu kazi za Taifa hasa vijana tuliokuwa tunawategemea wanatoweka taratibu.

Asanteee.

By technically/JF