Jeshi la polisi: Tunafanya mazoezi kupambana na uhalifu

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, limeendelea na mazoezi yake kwaajili ya ukakamavu ili kujiweka sawa na kupambana na tatizo la uhalifu.


Akiezungumza na waandishi wa habari Kamishna wa polisi kanda ya Dar es salaam, Simon Siro, aliwatoa hofu wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi na zoezi hilo kwani halipo kwaajili ya kuwatisha bali lengo ni kupambana na wahalifu na majambazi.

“Eeh kimsingi ni mazoezi ambayo tunayafanya kupitia maeneo mbalimbali kwa maana kwamba lengo kubwa ni kuzuia uhalifu hilo ndo lengo la kwanza, la pili ni kupambana na uhalifu kwasababu tunapokuwa tunapita maeneo mbalimbali lolote linaweza kujitokeza, wahalifu wanaweza jitokeza”, alisema kamanda Siro.

Aliongeza kwa kutoa mfano wa matukio yaliowahi kutokea alisema, “matukio mengi unaweza kuona kama ya panya rodi yanatokea sana sana maeneo ya Mbagala, lakini tukaona kwanini tufanye mazoezi haya kimya kimya ni vizuri wananchi wa kaona jeshi lao wakaona ukakamavu wa askari wao.”

“Hata miaka ya nyuma tulikuwa tunafanya na wala hatuna nia mbaya kabisa kwamba tunatisha wananchi hapana hatuna lengo la kutisha tunafanya katika mazoezi yetu ya kawaida na lengo kubwa kuzuia uharifu kwenye maeneo kwasababu naamini mtu muharifu akiona polisi anapita anakimbia”, aliongeza .

Naye kamishna wa oparesheni wa mafunzo ya jeshi la polisi Nsato Nsazya, aliwataka wananchi wasikejeli mazoezi hayo na kusema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya hivyo kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia mitandao ya kijamii