Shetta asema ushindani uliopo kwenye muziki umemfanya aogope kutoa ngoma mbaya

Hit maker wa wimbo ‘Namjua’ Shetta amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao hawajawai kutoa ngoma mbaya katika maisha yake ya muziki.
prima

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Shetta amesema biashara ya muziki imefanya afanye muziki wa kushindana kila siku ndio maana kila akitoa ngoma anahakikisha ni kali.

“Shetta sasa hivi ni mfanyabiashara, muziki wangu ni bidhaa adimu ndio maana mimi sijawai kutoa ngoma alafu isifanye vizuri, ni hit baada ya hit na ndo maisha yangu kwa sasa, na nitaendelea kufanya hivyo,” alisema Shetta.

Rapper huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kubiria surprise ya wimbo wake mpya baada ya ‘Namjua’ kufanya viruri.