Mwaka 2016 nilikuwa najiimarisha kwenye biashara, 2017 narudi rasmi kwenye filamu – Nisha


 Msanii wa filamu za vichekesho Salma Jabu aka Nisha amedai mwaka uliopita alifanya filamu chache na kuutumia muda mwingi kwenye kujiimarisha zaidi katika biashara.

Muigizaji huyo ambaye ni mfanyabishara wa vipodozi pamoja na nguo, amedai alikuwa anaweza mazingira ya biashara zake safi kwa kuwa anaamini hawezi kuigiza kwa miaka yote.

“Hakika 2016 ulikuwa ni mwaka wangu wa kufanya biashara tofauti na movie, 75% nimefanya biashara huku movie nikafanya 25% na yote hayo nilifanya ili kuweza kuweka msingi imara wa kujiingizia kipato bila kutumia ‘UNisha’ maana naimani kuna maisha baada ya haya na umri unasonga,” aliandika Nisha kupitia Instagram.

“Mwaka mpya 2017 ni mwaka wa kuziba pengo la filamu nikiwa na Nishasfilmproduction. Ahsante Mungu aliye mwema kwenye biashara ndoto kubwa nliyokuwa naiwaza tangu mdogo soon inaenda kutimia ikifika juu. No time to waste and drama zimeishia hapa.,” aliongeza Nisha.

Pia muigizaji huyo amewataka mashabiki wake wa filamu kusahau skendo zote zilizotokea mwaka 2016 huku akidai zilikuwa ni mbinu za kibiashara.

Disemba 2016 muigizaji huyo alidai kupewa mimba na mwanaume ambaye hakumtaja na baadaye kukataliwa.
Moja kati ya biashara za malkia huyo wa filamu