Hii Ndio Barua Nzito Aliyoandika Shamsa Ford Kwa Mumewe Ambaye Amehusishwa na Kesi ya Madawa ya Kulevya

Hakika ukipata mwanamke Kama huyu usimuache... Na huu ndio ujumbe wa shamsa kwa mumewe .


Shamsa Ford ameandika Haya:

Nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.

Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati .Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa..

Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani. Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani in shall ah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi..