HII NDIYO KAULI YA BABA YAKE DIAMOND PLATINUMS KUHUSU DIAMOND NA DARASSA

BABA wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Abdul Jumaa amefunguka kuwa Mwanamuziki, Shariff Thabeet ‘Darassa’ licha ya watu kusema yupo juu lakini hawezi kumshinda au kufikia levo alizopo mwanaye.Akichezesha taya na Mikito Nusunusu, baba Diamond alisema licha ya watu wengi kuvutiwa na Wimbo wa Muziki wa Darassa lakini hawezi kumshinda mwanaye huyo kwa sababu ni wimbo huo mmoja tu ndiyo uko kwenye chati kitu ambacho ni tofauti na Diamond ambaye anazo nyingi zinazofanya vizuri.“Diamond ni mpiganaji sana na ana mbinu nyingi kwenye suala zima la muziki wake ndiyo maana kila siku anazidi kuwa juu na kujulikana mataifa mbalimbali, wanaosema Darassa atampita au kumfikia Diamond alipo wanajidanganya, hawezi hata kwa nusu yake,” alisema baba Diamond