Mbasha, Miss TZ Mapenzi Mubashara...!!!!!

Baada ya kuficha uhusiano wao, Mwimbaji wa Gospo Bongo, Emmanuel Mbasha na Mshiriki wa Miss Tanzania 2008, Jacqueline Chuwa, sasa siyo siri tena kwani Wikienda lina picha zao mubashara wakiwa kwenye mahaba niue. Mtu aliyevujisha picha hizo, aliliambia Wikienda kuwa, Mbasha na Jack kwa sasa hawajifichi tena kwani wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali kama kanisani, sehemu za starehe na hivi karibuni walikuwa wakijiachia Siku ya Wapendanao huku wakiwa kwenye mavazi rasmi ya wapenzi.

“Naona wameamua kuweka mambo mubashara kabisa kwa sababu Mbasha ameshasarenda kwa aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha maana sasa ni malavu kwa kwenda mbele. Ukikutana nao hata hawajifichi baada ya Wikienda kuwaweka hewani,”

kilimwaga ubuyu chanzo chetu. Baada ya kupata ubuyu na picha hizo kutoka kwa sosi, mwanahabari wetu alimwendea hewani Jack ambaye muandaaji wa Shindano la Miss Tanzania mkoani Kilimanjaro ambapo alifunguka kuwa, hapendi kuzungumzia kiundani mambo yake ya uhusiano lakini anachojua ni kwamba, yeye na Mbasha ni marafiki na muda ukifika, kama kuna kinachoendelea ataweka wazi kila kitu. “Muda ukifika nitaweka wazi kila kitu kama kuna mambo ya ndoa na uchumba, wala msiwe na wasiwasi ninyi mtaona tu, suala hilo huwa halina kificho,” alisema Jack kwa bashasha.

Alipotafutwa Mbasha simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu pamoja na kwamba ulionesha kupokelewa. Wiki mbili zilizopita, Wikienda ndilo lilikuwa la kwanza kuripoti juu ya uhusiano wa Mbasha na Jack huku wawili hao wakija juu lakini sasa mapenzi yao siyo siri tena.