Msanii Wema Sepetu ajiunga na CHADEMA kutoka CCM

Habari: Miss Tz 2006, Wema Sepetu na familia yake watakuwa na Press Conference Saa 5 asubuhi nyumbani kwao Sinza-Meeda.

Waandishi wote wanakaribishwa.

Hiyo ndiyo meseji ya kutoka kwa akina Wema wenyewe kwenda kwa waandishi Asubuhi hii.

=======

Wema Last.jpg

Update: 1337hrs: Bado anasubiriwa Wema Sepetu hajafika, wanafamilia wengine akiwemo Mama yake na Baadhi ya viongozi wa CHADEMA ndo wapo.

Wema Amewasili na Kuanza Kuongea kama ifuatavyo:

⁠ ⁠Mama wema: Habari za mchana, nawakaribisha

⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Kwa jina naitwa Wema Sepeti Isack Abraham
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Naomba mnisamehe kwa kufika kwa kuchelewa
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Sitakuwa na mengi ya kuongea, nataka kutoa tamko moja kutoka kwa Wema mwenyewe
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Nimewaiteni hapa kuja kutamka rasmi kwamba hivi sasa nataka kuhamia Chadema kutoka CCM
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Sio kwa tuhuma zinazonikabili bali nmefanya maamuzi kama mtu mwingine yoyote

⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Nyote mnajua nlikuwa kada wa ccm na nmepigania chama kwa uwezo wangu wote
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: 2015 niligombea ubunge viti maalum Singida na kura hazimutosha na sikufa moyo
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Marehemu baba yangu alikuwa kada nguli wa CCM na alipata kuwa hadi mshauri wa Zanzibar, Waziri na Balozi wa Urusi. Amekufa akiwa CCM

Wema:
 Nimetuhumiwa hivi karibuni, wakati najitoa kwa hali na mali ndani ya CCM na nliamini hawatanitupa na haina maana kwamba nilitaka kubebwa hapana
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Kilichotokea kwangu kilikuwa ni uonevu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Nimetafakari sana kwanini hili limetokea
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Kama mwanachama kimenivunja moyo. Tenda wema uende zako usingoje shukurani

Wema: Mimi naamin katika demokrasia. Nmefanya reseach yangu na hata wakati wa kampeni CHADEMA ilitupa tabu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠CHADEMA inapigania demokrasia na mimi nataka uhuru wa watu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Ningejua mapema ningeniunga CHADEMA zamani. Najilaumu sana kuchelewa kujiunga CHADEMA

Wema:
 Bado sijachelewa kufanya maamuzi. Na hii najua nimeingia kwenye vita na naamini watu wengi wapo wananiunga mkono
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Dola ifanye kazi zake na kifuata sheria kama dola. Ila wazingatie haki za binadamu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Naamini ndani ya CHADEMA tunaweza kuleta mabadiliko nchini
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Kwa kupitia nguvu ya CHADEMA tunaweza pata ule uhuru tunaoupigania.

Tangu leo mimi sio mwanachama wa CCM. Mimi na mama tulikuwa wanachama hai wa CCM

Kwa upande wake mama Sepetu, alikuwa na haya ya kusema;

Mama Sepetu :Mmekuwa mnasema natoa mapovu,mimi sitoi mapovu

Mama Sepetu :
Uchungu wa mwana aunuae mzazi
Mama Sepetu :Nmehangaika sana mwanangu alipowekw ndani

Mama Sepetu :Ningejua mapema ningeniunga chadema zamani. Mama Sepetu :Najilaumu sana ku helewa jiunga chadema.

Mama Sepetu :Hakuzungumza yeye mimi sasa ndo nguli nazungumza

Mama Sepetu :Ametuhumiwa sana. Amekaa sero hamjamuona mwanangu akiwa alosto

Mama Sepetu :Hamna kiongozi wa ccm alokuja kuniuliza kulikoni

Mama Sepetu :Mpaka usiku walikuwa wanafuatwa mahabusu na makonda

Mama Sepetu :Haki za binadamu hazimuzingatia, watu wanaua wanapewa dhamana

Mama Sepetu :Lakini yeye kahangaishwa chana

Mama Sepetu :Mimi ni mkt wa ccm tawi la nzasa kata k/nyama tulikuwa na kura nyingi 2015

Mama Sepetu :
Wengi hataki kuzungumza wanauguliwa sana

Mama Sepetu :Sisi ni watanzania tumepanwa tupo kwenye kitanzi

Mama Sepetu: Mimi kama mama nmesema siwezi kuteswa na mwanangu kudhalilishwa tukiwa chama cha mapinduzi

Mama Sepetu: Mwanangu amezunguka na ccm anainadi nchi nzima

Mama Sepetu :Tangu leo mimi sio ccm tena. Na ntatembea nchi nzima kukinadi chama cha demokrasia na maendeleo

Mama Sepetu
 :Nashangaa chadema hawatupi kadi zao.

Mimi ni mwenyeji wa Singida. Baba katuacha tupo 72. Naenda kupokea kadi za CCM Singida na wote wameahidi kuhamia chadema

Wema: Naomba maswali matatu yanayohusiana na mimi kuhama

Swali: Unaidai CCM?

Majibu ya Wema: Wasanii wengi ikiwemo mimi nawadai, nikianza kuzungumzia madeni watasema ni kwa sababu tumehama. Mimi na wasanii wengine tunawadai CCM lakini wanatujibu tukamdai Kikwete rais mstaafu.

Mariam anauliza swali kuhusu voice note

Majibu: Mimi siku nyingi nimezima simu yangu, sijui wala sijaangalia kitu gani kimezungumzwa. Japo kuwa nmesikia kwamba kuna sauti. Siijui kabisa

Mimi simu yangu ina matatizo, siwezi kuisikiliza hiyo sauti, mlioisikia ni nyinyi sio mimi

Steve ni mtoto wangu sasa hiyo sauti yangu na Steve siijui

Wala sijawahi kuisikia ila nina mpango wa kuisikiliza simu ikipona

Je huu uamuzi ni wa hasira?

Wema: Hapana sio wa hasira, nimepata hasira kura za viti maalum na ndo ningehama. Hadi hapo CCM ilipo ina jasho langu na nguvu zangu. 
Nimeonewa na imefanywa nijisikie mnyonge ndani ya chama

Nilijitoa ikibidi nife. Nilipoenda Zanzibar wanachama wa CUF walitaka kunimwagia tindikali kisa mimi ni wa CCM. Walinimwagia michanga. Hiyo yote ni katika harakati za kuitetea CCM

Leo chama ndo kimefanya nipitie yote Haya

Mapenzi ni nipe nikupe, mapenzi yakiwa ya upande mmoja sio mapenzi

Je chadema wamekununua? 

Majibu: 
Chadema hawajanipa hata sh 10. Ni mapenzi yangu tu. Hayo mambo ya fedha tumezoweshwa kwa sababu chama cha mapinduzi ndo mtindo wao.

Huu ni uamzi mgumu sana, na mimi nikishasema basi ni basi. Sirudi nyuma.

Chadema wanapigania demokrasia. Tanzania yetu imeanza kupoteza demokrasia kwa kiasi kikubwa.

Sijaingia kwenye mitandao. Natamani niingie na kutoa kale kapicha ka CCM nilichokipost tatizo sijapata muda wa kuingi kwenye mitandao. 
Kama ni vita nimeshavaa magwanda nipo tayari kupigana 
Chadema wamenipokea kwa mikono miwili 

Swali: Kuna mtu mkubwa una bifu naye, CCM unafanyiwa hivi, je chadema si itazidi?

Kwanza kabisa sina bifu na mtu yoyote kutoka CCM 

Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge 

Kumbuka mimi nina kesi mahakamani, tunachopigania ni uhuru na demokrasia. 

~MWISHO~