Za Chini ya Kapeti...Diamond Hana Furaha na Zari,Makubwa Yaanikwa Juu ya Maisha ya Wawili Hao Ndani ya Nyumba..!!!!


Taa nyekundu inamuwakia staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya kubainika kuwa hana furaha na mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady  ’, twende pamoja hapa chini.

RAFIKI AMWAGA UBUYU

Mmoja wa wanafamilia wa Diamond (jina tunalo), ameibuka na kuvujisha ubuyu wa motomoto kwa Wikienda kuwa, jamaa huyo hana furaha na Zari kwani ameanza kuona kuwa huko tuendako uhusiano wao hauna mwisho mzuri.

AMEANZA KUSHTUKIA?

Mtu huyo wa karibu zaidi na Diamond ameeleza kuwa, staa huyo naye ameanza kuhisi kwamba huenda Zari hakumpenda kama alivyo na zaidi alifuata ‘chapaa’ ambapo anaweza kusepa zake muda wowote endapo fedha zitampiga chenga staa huyo wa Wimbo wa Marry You aliomshirikisha Ne-Yo wa Marekani. “Iko hivi, Diamond mwanzoni alikuwa anachukulia poa lakini nafikiri sasa hivi inafikia wakati hata yeye kengele ya hatari imeanza kugonga. Nafikiri ni kwa sababu sisi tunavyomshtuashtua  kwamba awe makini naye maana anaonekana ni mjanjamjanja sana.

“Kwa taarifa tulizozipata, hata kule Afrika Kusini, inaonekana alimwagana na yule mumewe (Ivan Semwanga) kwa sababu ya kuvuna alichokuwa amekitaka, hivyo mara nyingi sana hata mimi nimekuwa nikimueleza Diamond awe makini sana katika eneo hili,” alisema mwanafamilia huyo.

WEMA NDO’ MPANGO MZIMA

Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, Diamond alikuwa sahihi alivyokuwa kwenye uhusiano na mlimbwende matata Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kwani ni mtu ambaye alikuwa anamfahamu vizuri historia yake na mwenye mapenzi ya dhati. “Si unajua Wema akipenda huwa anapenda kweli? Ndo’ maana licha ya kuwa miaka ya karibu minne imepita  sasa tangu waachane, lakini Diamond bado anaonekana kulikumbuka sana penzi la Wema.

“Anauona upendo wa kweli kwa Wema licha ya kuwa walipishana kwa namna moja au nyingine. Wema hakuonesha kwamba anamhitaji kwa ajili ya fedha. Ndiyo maana alianza na Diamond hata akiwa bado fedha hazimchanganyia kivile,” alisema ndugu huyo.

USHAURI WA BURE

Jamaa huyo alisema kuwa, wao kama familia, ingawa si busara sana kumshauri mtu kuhusiana na suala zima la mapenzi, lakini wameona si vibaya kama watampa tahadhari ili aweze kuchuja mbivu na mbichi. “Tunataka ajue kama anaendelea kuishi naye, aishi naye kwa staili gani ili asiumbuke baadaye itakapotokea ameshuka kimuziki.

“Hatumwambii amuache, lakini  tunataka ajue kwamba tunasikia mengi yanayomhusu. Inasemekana Zari suala la kumzalia mwanaume ili aweze kutimiza matakwa yake siyo ishu.

‘ALIMPIGA’ IVAN?

“Kwa Ivan (mume wa zamani wa Zari) alikuwa mpole. Akavuna mkwanja wa kutosha ambao ulimwezesha kufungua maduka na kumiliki shule na vyuo Afrika Kusini ikiwemo na kuweka makazi katika nchi ambayo si yake.

“Nini hawa watoto wawili wa Diamond? Ivan alimzalia watoto watatu. Na ninasikia jamaa (Ivan) kuna wakati mambo hayakwenda vizuri, wakamwagana. Huku na huku ndiyo akajitokeza Diamond. Kipindi hicho Diamond ndiyo alikuwa ameanza kulishika soko la muziki Afrika Mashariki na mshiko nao ulikuwepo.

NI MJANJAMJANJA?

“Ukitazama kwa makini utaona namna ambavyo Zari ni mjanjamjanja, alichungulia Bongo, akaona anaweza kumtumia Diamond kupiga hela. Akaja na wazo la Zari All White Party, akaona isingekuwa rahisi kwa mtu mgeni kama yeye kuja kufanya tamasha nchini, akamtumia Diamond, akapiga mkwanja. Akatambaa,” alisema jamaa huyo.

NI KATILI?

Rafiki huyo alizidi kuweka bayana kuwa japo wao hawawezi kuhukumu moja kwa moja lakini kupitia matukio hayo, wanashindwa kumuwekea asilimia mia moja kwamba si mkatili. “Sisi tuko naye karibu. Tunamuona hata macho yake yanasema nini lakini hatuwezi ‘kujaji’ moja kwa moja ila kuna vitu tunaviona.

Mfano mdogo sana, kwenye ile Arobaini ya Nillan (mtoto wa pili wa Diamond), kuna jambo Zari alilifanya, tulishangaa sana. “Lilikuwa na viashiria fulani vya ukatili maana alimyakua Nillan kama vile ameshika bawa la kuku. Kitendo kile kilizua minong’ono sana kiasi ambacho wengi walitafsiri kwamba ni kitendo cha ukatili,” alisema rafiki huyo.

ZARI ANASEMAJE?

Wikienda lilifanya jitihada za kumsaka Zari bila mafanikio kwa kwenda nyumbani kwa Diamond zaidi ya mara tatu lakini walinzi walikataa kuruhusu mzazi mwenziye huyo wa Diamond kufanya mahojiano.

ALIWAHI KUFUNGUKA…

Hata hivyo, huko nyuma Zari alishafikishiwa habari kwamba Wabongo wamemshtukia kwamba ni mpigaji ambaye anatumia kigezo cha uhusiano kama silaha ya kuvuna fedha (gold digger) ndipo mama huyo wa watoto watano alipofunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram: “When people call you a gold digger show them how you dig, too much money out there for all of us. Why hate? Stop BITCHCRAFTY it’s the 21st century,” aliandika hivyo akiwa anamaanisha kuwa hajali kuitwa mwizi wa mapenzi na kama akiitwa hivyo, anawaonesha kwa matendo namna gani anavuna fedha kwa ajili yao wote hivyo watu waache kupiga majungu katika karne hii ya 21.

Alipotafutwa Diamond kuhusiana na ushauri huo aliopewa, aliomba yeye asiwe mzungumzaji kwa sasa. KUMBUKUMBU Diamond kabla ya kutua kwa Zari, alishawahi kuwa na uhusiano na warembo wakali Bongo akiwemo mwanamitindo Jokate Mwegelo na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’ ambao wote walizidiwa nguvu ya umaa rufu na uhusiano wake na Wema.