AUDIO: Wananchi wavamia Shule na Kubomoa Vyoo Vya wanafunzi

Wananchi wa mtaa wa Ramadhani Mkoani Njombe wameamua kubomoa vyoo vya shule baada ya kuikabidhi kamati ya shule matundu 14 ya vyoo walivyovijenga kwa nguvu zao kwa asilimia 100 kwa madai kuwa watoto wao kuendelea kutumia vyoo vya zamani ni kuendelea kuhatarisha afya za watoto

Wamefikia kuvunja vyoo hivyo baada ya taarifa kutoka ofisi ya mkurugenzi kuagiza vyoo vya zamani kuendelea kutumika mpaka uzinduzi utakapo fanyika na mbio za mwenge ifikapo mwezi wanne mwaka huu.

Muda mfupi baada ya mwenyekiti wa mtaa wa Ramadhani kuwatangazia wananchi kuwa wananchi wangali wanatumia vyoo vibovu licha ya kamati ya shule kukabidhiwa rasmi wananchi wakaungana na kwenda kuvunja.

Kutokana na tukio hilo Afisa elimu msingi halmashauri ya mji Njombe wakishirikiana na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ramadhani Efraimu Kyando wakalazimika kuripoti kituo cha polisi Njombe ambapo mwenyekiti wa mtaa huo akalazimika kutoa maelezo ya kwanini aliruhusu wananchi kuvunja vyoo chakavu.

TAARIFA ZAIDI NA MWANDISHI WETU PROSPER MFUGALE, MSIKILIZE KWA KUBONYEZA PLAY HAPO CHINI