KAJALE AMUWEKA WAZI MCHEPUKO WAKE


Ubuyu mtamu wa Wikienda! Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ anadaiwa kupata bwana mpya ambaye kutwa, kucha amekuwa akimposti kwenye mitandao ya kijamii hasa Snap Chat akitamba kuwakomesha wambeya wa Instagram.

Kwa mujibu wa sosi makini, Kajala kwa sasa ana mpenzi mpya ambaye amekuwa akitesa naye kwa kutupia mapichapicha mitandaoni akijiachia kwa kufanya naye mazoezi ‘gym’.

MSIKIE SOSI

Sosi: Hivi jamani Wikienda mna ubuyu mpya mjini?

Wikienda: Ubuyu upo wa kila aina hapa sema tu wewe kama una wa kwako sisi tutaufanyia kazi na kuurusha hewani.

Sosi: Ubuyu mpya ni kwamba sasa hivi Kajala ana bwana mpya ambaye anatokana naye, unaambiwa watu hatunywi maji.

Wikienda: Ni bwana gani huyo? Je, ni staa au ana jina mjini?

Sosi: Nasikia ana asili ya Kisomali. Kuna watu wanasema anacheza kikapu maana ameenda hewani. Fuatilieni mtapata ubuyu freshi kabisa kabla hamjapigwa skupu.

PICHA ZA SNAP CHAT

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Wikienda lilianza kunyapianyapia ambapo lilielezwa kuwa, kulikuwa na picha za Kajala na jamaa huyo ambazo ziliibwa kwenye Snap Chat na wambeya kisha kuzitupia kwenye Instagram, jambo lililomfanya Kajala aumbuke kwani hakuwa na namna zaidi ya kupiga kimya.

WIKIENDA KAZINI KUICHIMBA

Baada ya picha hizo kutupiwa Instagram, Wikienda lilizama kazini kuchimba ukweli ambapo lilibaini moja kwa moja kuwa Kajala na bwana huyo ambaye jina lake bado lipo kwenye mabano ni wapenzi kutokana na jinsi mwanamama huyo anavyotupia picha zao.

Ilibainika kuwa, Kajala amekuwa akitupia picha nyingi zikiwaonesha wakiwa wamekumbatiana na kushikana viuno na maeneo mengi

BETHIDEI YA JAMAA

Hata hivyo, siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa jamaa huyo hivi karibuni, Wikienda lilibaini kuwa, jamaa huyo ni mtu wa Kajala kwani staa huyo alitupia picha za jamaa huyo akimtakia heri ya kuzaliwa ambapo aliandika maneno yaliyoweka wazi kuwa ni  mpenzi wake ambayo yalisomeka:

“Happy birthday my heart beat!” Kama hiyo haitoshi, mmoja wa watu wa karibu wa Kajala alitupia picha za wawili hao akimuwishi jamaa huyo heri ya kuzaliwa, jambo lililofunua kila kitu kwani wana ubuyu walifafanua kuwa, aliyezaliwa ndiye bwana mpya wa Kajala.

Baada ya ubuyu huo kukaa kwenye kilo, Wikienda lilianza kusaka mzani wake kwa kumtafuta Kalala kwa njia ya simu ambapo hakutaka kuzungumza zaidi ya kuomba habari hiyo isiandikwe.

MSIKIE KAJALA

“Naomba usiandike lolote juu ya habari hiyo,” aliomba Kajala, ombi ambalo lilitupiliwa mbali. Kama hiyo haitoshi, Wikienda halikuishia hapo kwani siku iliyofuata Kajala aliombwa tena kuzungumzia ubuyu huo ambapo alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno ulioonesha umesomwa lakini haukuwa na majibu.

NENO LA MHARIRI

Kama Kajala amepata mchumba inabidi ajitafakari kwani ni katika kipindi ambacho mumewe, Faraji Agustino ametoka gerezani na wengi walitarajia aungane naye tena kwa ajili ya kusongesha gurudumu la maisha kwa sababu ndoa yao bado haijavunjika.