LEILAH RASHID AMTIBULIA MZEE YUSUF KWA MASHEHE

Leilah Rashid. 
Alhaji Mzee Yusuf ambaye zamani alikuwa muimbaji wa Muziki wa Taarab, anaendelea na jitihada zake za kuitangaza Dini ya Kiislam, lakini malalamiko yamekuwa yakielekezwa kwa mkewe, Leilah Rashid ambaye inaonekana kama ameweka ngumu kuacha muziki.
Mashehe.
Mtu wa karibu wa Mzee Yusuf alilitonya gazeti hili kuwa, kitendo cha Leilah kuendelea kufanya mambo ya kidunia hakiwafurahishi viongozi wa dini na wamemtaka Mzee kufanya uamuzi mgumu.
“Kidini inakuwa haileti picha nzuri endapo wewe utakuwa unajikita kwenye ibada na mkeo yupoyupo tu, ndiyo maana tunaambiwa kuwa, siku ya kiama wake na watoto wetu watakuwa mtihani mkubwa kwetu.
Leila Rashid na mwanaye.
“Tunatakiwa kuwafanya watoto na wenza wetu wafuate maamrisho ya Mungu, sisi tukijikita kwenye ibada na wake zetu na watoto wetu wakawa wanafanya yale ya kumkera Mungu, siku ya kiama adhabu itakuwa kubwa.
“Ndiyo maana baadhi ya mashehe wanaokuwa karibu na Mzee Yusuf wanajisikia vibaya kuona mke wake anaendelea kufanya muziki,” alidai mtoa habari huyo.
Hata hivyo, wakati f’lani Mzee Yusuf alipoulizwa ana mkakati gani wa kumfanya mkewe aungane naye katika kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, alisema kuwa anaamini siku moja itakuwa hivyo kwani hata yeye ilimchukua muda kumrudia Mungu wake.
Mzee Yusuf.

Naye Leilah hakuweza kupatikana kwenye simu yake lakini aliwahi kumwambia mwandishi wetu kuwa, hawezi kuacha muziki kwa haraka hivyo ila siku ambayo Mungu atapenda aache muziki, ataacha. Leilah ambaye ni mke wa pili wa Mzee Yusuf ni kati ya waimbaji mahiri na tegemeo wa Bendi ya Taarab ya Jahazi ambayo huko nyuma mmoja wa wakurugenzi wake alikuwa mumewe Mzee Yusuf.