Mikataba ya Ozil , Sanchez Yapigwa Stop Arsenal

 Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema mazungumzo ya mikataba ya Alexis Sanchez na Mesut Ozil yamesimamishwa kwa muda.

Wachezaji hao walikuwa kwenye mazungumzo ya mikataba mipya na timu hiyo, lakini kocha huyo amesema mazungumzo hayo yataendelea mwishoni mwa msimu.

Wenger amesema hakuna mazungumzo yatakayofanyika kuhusu mikataba hiyo hadi mwishoni mwa msimu.

“Tumeanza kufikiri kuhusu jinsi tunavyoweza kumaliza msimu huu na mazungumzo ya mikataba ya wachezaji hao yatafanyika mwishoni mwa msimu.

“Kwa sasa tuna mambo mengi, hivyo ni vyema tukakaa mwishoni mwa msimu huu ili kumaliza mambo yote haya,” alisema Wenger.