MREMBO JIKE SHUPA AJUTIA MITUNGI

MREMBO ambaye chimbuko lake ni Video Queen Bongo,jike shupa amesema anaichukia sana pombe kwani inamfanya vibaya, kila anapokunywa, anafanya vitendo ambavyo sio sahii kwenye jamii na kumletea madhara.
Akizungumzia jinsi pombe inavyompa matokeo mabaya, Jike Shupa alikumbushia tukio la hivi karibuni baada ya picha kuvuja zikimuonyesha akipigana mabusu na mwanamke mwenzake kutokana na ulevi.

“Kwa hivi sasa pombe naiona chungu sana kwa sababu imeniletea matatizo sana maana hata jamii yangu hainielewi kabisa na ninaonekana mtu wa hivyo inabidi niipe likizo kabisa pombe kwa sasa,” alisema Jike Shupa.