MREMBO LULU DIVA AHONGWA GARI MPYA AINA YA JEEP..SHUHUDIA HAPA

BAADA ya kutajwa kwenye orodha ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya na kuachiwa baada ya kushikiliwa kituo cha polisi ‘Sentro’ kwa muda wa wiki moja, Mwanamuziki wa Lulu diva amehongwa ndinga jipya aina ya Jeep.
Imeelezwa aliyemhonga ni mwanaume wake anayemuweka mjini kwa sasa.
Rafi ki wa karibu na mwanamuziki huyo aliiambia Mikito Nusunusu kuwa Lulu Diva tangu apate misukosuko hiyo mpenzi wake amekuwa naye karibu sana kiasi ambacho ameamua kumhonga ndinga hilo la bei mbaya ambalo ndilo analotamba nalo mitaani huku akiwa hana kadi ya gari hilo.
“Unajua Lulu tangu apate misukosuko mpenzi wake ameongeza mapenzi zaidi hata hilo gari alilomhonga ni kwa ajili ya kumfanya ajisikie vizuri na kusahau kama alipata shida hiyo kubwa lakini bado kuna utata kwenye kadi ya gari,” alisema rafi ki huyo.

Mikito Nusunusu ilifunga safari mpaka nyumbani kwa Lulu Diva ambapo ilikuta gari hilo likiwa limepaki nje na alipoulizwa alisema; “Ni gari langu lakini pia hata baby analitumia kama analihitaji na gari hili ndilo lilikuwa la ndoto yangu, kuhusu kadi hiyo ni siri yangu siwezi kuzungumzia,” alisema Lulu Diva