Noma Sana..Dude Atoa Yake ya Moyoni Kuhusu Aliyoyafanya Rais Magufuli Kwenye Mkutano wa CCM,Adai Alishangazwa na ...!!!!

BAADA ya baadhi ya mastaa wa filamu kuungana na wanachama wa CCM kwenye Mkutano Mkuu uliofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni, msanii Kulwa Kikumba ‘Dude’ alijikuta akipagawa baada ya Rais Dk. John Magufuli kuwapongeza wasanii.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Dude alisema Rais Magufuli alimfurahisha kwani ni kwa mara ya kwanza wasanii waliofika kwenye mkutano huo kila mmoja alitambulishwa kwa majina yake tofauti na miaka mingine huku akiwapongeza kwa kuungana nao katika mkutano huo.

“Nilifurahi sana kwa kweli maana kule kwenye mkutano Rais Magufuli alitupa kipaumbele na kutupongeza kwamba siyo kama wale wengine waliopata matatizo kidogo na kukimbia kwenye chama huku tukiahidiwa kuwa serikali itatuandalia sera nzuri ya filamu ili kuvuta wawekezaji,” alisema Dude.