Rais Magufuli azidi kuiandama mitandao ya Kijamii..


Akiongea leo wakati anaapisha wateule wapya Ikulu. Amesema mitandao yetu ni ya ovyoovyo na inaandika mambo ya ajabu ajabu.

"Jana nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuwa eti Mwakyembe hawezi kuja kuapishwa, na mimi nilikuwa nasubiri asifike nione. ''Sasa si huyu hapa amefika"

Ameongeza kuwa..... "Jana kuna mwingine kapost Kinana kuongea na waandishi wa habari kesho, wakati ukweli Kinana nimemtuma India Kwa siku kumi na mbili"

Amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari kwa kuzipa nafasi habari mbaya mbaya tu, "mfano kuna tv habari za migogoro ya wafugaji ndio wanaipa nafasi kubwa zaidi, amesema hayupo tayari kuvumilia hayo mambo.

Ameshangaa magazeti ya leo kujaza mbele picha ya mtu mmoja, na hata kurasa za ndani kujaza habari hiyo hiyo.

Amemwambia Mwakyembe akasimamie kwa umakini hasa tasnia ya habari, amesema hayupo tayari kuona nchi ikichezewa..l

Ameshangaa kutangaza kutoandika habari za mtu, wakati huo huo wanaandika mbaya tu.... "Kama hamtaki kumwandika si masiandike yote mazuri na mabaya"