Rais Magufuli na mkewe wawasili mkoani Dodoma

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amewasili Mkoani Dodoma ambako pamoja na mambo mengine ataongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa, Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi.

Mhe. Dkt. Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM ataongoza kikao na mikutano hiyo kuanzia tarehe 10 - 12 Machi, 2017 Mjini Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli waliwasilijana katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma akitokea Mkoani Morogoro ambako jana tarehe 06 Machi, 2017 alizindua uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere.