Rais Mhe. Dkt. Magufuli Avitaka Vyombo vya Habari Kuweka Mbele Uzalendo...!!


Rais wa Tanzania Mh Dkt. John Magufuli amevitaka vyombo vya habari nchini kuweka mbele uzalendo kwani wao wana mchango mkubwa katika kuliinua  ama kuliangamiza taifa.

Mhe. rais ameyasema hayo alipokuwa  akizungumza  Ikulu bada ya kupokea hati za utambulisho za mabalozi na kuwaapisha viongozi mbalimbali  akiwemo waziri mpya wa habari utamaduni sanaa na michezo Mhe. Dkt. Harrisoni Mwakyembe.

Rais akasema inashangaza kuwa mataifa ya nje  yanathamini na kuheshimu jitihada zinazofanywa na serikali na ndio maana hata rais wa benki ya dunia alikuja nchini kwa mara ya kwanza lakini baadhi ya wananchi hawaoni jitihada hizo, wanabeza.

Kiongozi huyo  akawataka viongozi kutovunjika moyo wafanye kazi na wananchi waache kulalamika bila ya kutoa ufumbuzi wa hayo malamiko yao.

Katika hafla hiyo alikuwepo makamu wa rais mama Samia Suluhu Hassani ambaye alisema kila mtu anapaswa kufanya kazi huku ,kaimu jaji mkuu Prof. Ibrahim  Hamis Juma akiwataka viongozi kuzingatia maadili.