Tiba kwa Mpenzi Anayekojoa Kitandani...!!!


Ni matumaini yangu mpo salama,
Naamini kuna watu humu wamewahi kuachwa au kuachika kisa kuwa na tabia ya kujikojolea kitandani wakati wa usiku,

Baadhi ya wanandoa wanapitia kero hii sana sema huhifadhiana siri kwa sababu walisha kula kiapo cha pingu zamaisha,
Baadhi yao uzalendo huwashinda pale chumba kinapoanza kunukia kibeberu beberu na kuamua kuvunnja ndoa zao,

Usifadhaike ,

Kama una mpenzi, ndugu, jirani au mtoto mwenye tatizo la kukojoa kitandani leo ninamwaga tiba yake hapa ili mkapate kuwasaidia,

TIBA,
Ufuta mbichi (ambao hauja kaangwa),
Unapatikana sokoni, 
Baada ya kuununua upepete ili kuondoa mchanga na vumbi,
Baada ya hapo tafuna vijiko vinne vya ufuta kutwa mara tatu, tumia kuanzia siku tatu na kuendelea,
Utapona kabisa na itabaki kuwa historia,
Hii imewasaidia wengi sana,

Kwa leo naishia hapa,