Ukweli Ndio Huu..Watumiaji wa Mitandao na Watanzania Tumelishwa Tango Pori Kuhusu Mtoaji Bastola kwa Nape Pale Protea..!!!


Najua wengi mtashtuka na wengine kunipinga hadi kunibishia ila kwa ushahidi wa jicho la Tatu na la msaada wa Wataalam wa Saikolojia na Wabobezi waliotukuka kwa Utambuaji wa Mtu / Watu yule Mtu tunayeambiwa kuwa ndiyo alimtolea Bastola Nape Nnauye pale Protea na ambaye picha zake zinasambazwa Mitandaoni siyo Mhusika halisi bali tumedanganywa.

Ili kuweza kuamini hili tafadhali hapo hapo ulipo itafute picha ile ya yule wa Protea kisha kwa umakini wako mkubwa kabisa huku ukiwa umetuliza akili zako zote ilinganishe na hizi picha zinazotembea Mitandaoni na utapata jibu.

Mbinu iliyotumika hapa ni ya Kijasusi zaidi na ya hali ya juu ambapo kuna Mtanzania mmoja anayeaminika yupo Ughaibuni na hupenda mno kukurupuka kuwalisha matango pori Watanzania na wapo wanaomuamini hivyo kilichofanyika kwakuwa anajulikana kuwa na ' kiherehere ' Watu wenye Kazi zao na waliobobea wakaamua kumtumia picha za Mtu anayeonekana katika Mitandao ili zisambae haraka lakini Mhusika Mkuu ( Mtoaji Bastola ) akiwa yupo mahala pengine na anaendelea na majukumu yake.

Nasisitiza tena kuwa tulieni na ziangalieni kwa umakini mkubwa hizo picha na mwishoni mtapata majibu kuwa tumelishwa matango pori na tumeshiba kabisa ila mchomoaji Bastola kwa Nape pale Protea kwa 100% siyo huyu mwenye picha tunazoziona Mitandaoni. Huyo Binti wenu wa Ughaibuni sasa hivi Watu wanampa taarifa za Uwongo ili kuweza kumuharibia na aonekane bure na nasikitika kwamba huu mtego hajaushtukia na kila mara anauvagaa tu.

Ijumaa Karim nyote