Yakufahamu Juu ya Urefushaji wa Maumbile ya Wanaume..!!!


Kwa ufupi
Makala ya juma lililopita ni mojawapo ya makala niliyopokea maelfu ya maswali kutoka kwa wasomaji, naamini kama tutakuwa pamoja mtapata majibu ya maswali yenu katika mfululizo wa makala tatu zijazo.

By Dk Shita Samwel

Juma lililopita tuliona sababu za wanaume kuwa na maumbile madogo ya uume. Leo tunaendelea sehemu ya pili, tutaona dondoo za kitafiti zenye kueleza ukweli wa maumbile ya uume.

Makala ya juma lililopita ni mojawapo ya makala niliyopokea maelfu ya maswali kutoka kwa wasomaji, naamini kama tutakuwa pamoja mtapata majibu ya maswali yenu katika mfululizo wa makala tatu zijazo.

Wanasayansi wengi wa tiba wametoa machapisho mengi ya kitafiti kuhusu urefu na upana wa uume nia na madhumuni ni kujibu swali juu ya wastani wa uume kwa wanaume wengi duniani ni upi.

Baadhi ya wanaume wamekuwa wakiishi kwa hofu na kukosa kujiamini katika uhusiano wao wakihisi kuwa wana uume ambao ni mdogo usioweza kumridhisha mwenza wa kike.

Hofu hiyo inawezekana ni kutokuwa na ufahamu sahihi juu ya maumbile yao yalivyo, wengi wanakosa taarifa sahihi kutoka wataalamu wa afya wenye uelewa wa jambo hili.

Hofu ya wanaume inaongezeka kila siku hasa kutokana na utitiri wa matangazo ya magazeti, mitandaoni, hadithi za vijiweni na matangazo ya waganga wa kienyeji mitaani wanaojitangaza kuwa na dawa na vifaa tiba vya kuongeza urefu na upana wa uume.

Dondoo zifuatazo zinajumuisha ripoti mbalimbali za kitafiti, ikiwamo yale yaliyochapishwa katika majarida makubwa na maarufu duniani ikiwamo ya Science today, Men’s health na British Journal of Urology international.

Asilimia 85 ya wanawake wanaridhika na urefu na upana wa maumbile ya uume wa wenza wao, ingawa wanaume wenyewe hawana uhakika wa jambo hilo, huku asilimia 45 ya wanaume wakiamini kuwa wana maumbile madogo.

Tafiti mbalimbali zilikuja na hitimisho kuwa wastani wa urefu wa uume ukiwa haujasimama, ukiwa katika hali ya ulaini ni kati ya sentimita 7 hadi 10 au inchi 2.8 hadi 3.9, urefu unapimwa kuanzia katika shina la uume mpaka katika kichwa.

Wakati kipimo cha mzunguko wa uume ukiwa haujasimama ni kati ya sentimita 9 hadi 10 au 3.5 hadi 3.9

Urefu wa uume unapokuwa umesimama ni kati ya sentimita 12 hadi 16 au inchi 4.7 hadi 6.3. Urefu wa mzunguko wa uume ukiwa umesimama ni kati ya sentimita 12 au inchi 4.7.

Dondoo nyingine ya tafiti inaonyesha kuwa wanaume wenye unene uliopitiliza na wenye umri mkubwa wengi wao wana “urefu mfupi” wa uume ukiwa umesimama.

Maumbile ya uume yanatofautiana kati ya jamii moja na nyingine, bara moja na jingine. Wanaume wanaotokea Asia wana maumbile madogo ya uume ukilinganisha na wanaume wa bara la Afrika.

Wanawake wengi huwa hawajali urefu na upana wa uume wa wenza wao, pengine ni kutokana na ukweli kuwa kufika kilele cha tendo kwa wanaweka si lazima kumuingilia, wanaweza kufika kileleni hata kwa njia nyingine hata kwa kutomaswa.

Daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama Ernst Grafenberg mwenye asili ya Ujerumani, ndiye mgunduzi wa sehemu ya kike ambayo ndio inaelezwa ina msisimko wa kipekee kuliko nyingine yoyote katika sehemu za kike.

Sehemu hiyo ijulikanayo kama G-spot ambayo ipo sentimeta 5.1-7.9 au nchi 2-3 tu kuanzia nje ya uke kuingia ndani.

Inaelezwa kuwa unaweza kuwa na uume mdogo lakini ukamridhisha mwenza wako na kumfikisha kileleni kutokana na sehemu hiyo huweza kusisimuliwa hata na uume mdogo.