Kumbe Mkuu wa Mkoa lazima awe na Digrii, Isome Hapa...


Siku mbili baada ya Mheshimiwa Angela Kairuki, Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kukabidhi ripoti ya Vyeti kwa Rais Magufuli na kusema "Uhakiki huu haujafanyika kwa viongozi wa Kisiasa ambao wako serikalini kama vile Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao mamlaka ya uteuzi ndio wanajua ufanisi wa kazi zao na pia katika Siasa suala ni kujua kusoma na kuandika." 


Hoja hiyo imezua mjadala mzito ambapo Wakili Msomi Peter Kibatala kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti nakala inayoonesha majukumu, na sifa za kilemu anatakiwa kuwanazo mtu wa cheo cha Mkuu wa Mkoa ikiwemo kuwa na elimu ya ngazi ya Digrii.