Mrembo Rayuu Afungukia Kuhusu ndoa yake Kuvunjika


BAADA ya madai kuzagaa kuwa ndoa yake imevunjika, msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ ameibuka na kueleza kuwa madai hayo yametokana na watu waliozoea kuona akimuuzisha sura mumewe mtandaoni lakini ameamua kusitisha tu na siyo kwamba ndoa haipo. 

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Rayuu alisema, awali alikuwa anapenda kumuanika mumewe kwenye mitandao ya kijamii lakini kutokana na maneno ya hapa na pale ya watu wasioitakia mema ndoa yake akaona bora asimuweke lakini ndoa yao ipo imara na hawafi kirii kuachana.

“Naweza kusema hii ndoa imenikuza, kwa maneno ya watu nimejifunza mengi kwenye hii dunia yaani utoto wote umeisha, wengi wanajadili kuwa tumeachana sababu hawaoni nikimuweka kwenye mitandao kama mwanzo, kwani nimegundua hakuna faida bali ni kujiletea matatizo yanayoweza kuvunja ndoa, japo kukosana ni kawaida kwenye mapenzi,” alisema.