Mume wa Shamsa Ford afunguka baada ya kudaiwa kumpigaShamsa Ford alidai kupigwa bila kukusudia wakati akiamulia ugomvi wa msichana wake wa kazi, lakini zipo taarifa zinasema majeraha hayo yametokana na kupigwa na mume wake Chidi Mapenzi baada ya kufumwa akinywa pombe. 

Ili kuujua ukweli wa tukio hilo Soudy amepiga story na Chidi Mapenzi na haya ndiyo aliyoyasema:”Siwezi kumpiga mke wangu. Wewe mwenyewe unanijua mimi siyo mgomvi. Nilitoka ofisini, nikamkuta mke wangu ameumia, nilipomuuliza nini tatizo, akanielezea. Nilipomuuliza unamjua mtu mwenyewe, akasema tumeyamaliza. Basi nikampeleka hospitali.” – Chidi Mapenzi.