Mwanamke Usafi Bibieh..Jifunze Jinsi ya Kuondoa Weusi Kwapani iIli Uwe Huru..!!!


Najua wengi wana tatizo la makwapa kuwa meusi tii hadi wanaogopa kuvaaa vijiguo wazi maana lol. Sasa hapa nakupa some tips zakuondoa huo weusi katika makwapa. Hapa ni njia 3 za kukusaidia; tumia ile iliyo karibu zaidi na wewe.

Baking Soda

Changanya baking soda na maji.
Weka au paka hapo kwenye kwapa jeusi
Acha kwa dakika 10 – 15
Osha na maji ya vugu vugu

Uwe ukifanya hivyo mara kadhaa katika wiki utaona tatizo lako linakwisha

Apple Cider Vinegar

Pakaa hiyo apple cider vineger
Baada ya dakika 5 futa na kitambaa cha cotton – usioshe na maji

Viazi ulaya

Kiponde ponde
Kisha pakaa uji wake katika kwapa
Acha kwa dakika 30 kisha osha vizuri

Haya nimekupa hizo tiba tatu tofauti kuondokana na kwapa jeusi please.