HII NI KUFURU: TAZAMA Kundi la IVAN la RICH GANG lilivyofanya Kufuru Mazishini Kwa Ivan #TAZAMA

Maajabu yanazidi kujionesha tu katika msiba huu wa Ivan. Leo tarehe 30 ndio siku ambayo Ivan kapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huko Kayunga Uganda sehemu ambayo ndio asili ya wazazi wake.
Katika eneo alilozikwa ndio sehemu ambayo pia ndugu zake wengine walizikwa. Tukio hilo la mazishi lilihudhuriwa na mamia ya watu wengi wao wakiwa na majonzi makubwa kwa kumpoteza Ivan.
Miongoni mwa matukio yaliyowaacha midomo wazi watu ni kitendo cha matajiri wa kikundi alichokuwa akikiongoza cha RICH GANG kuzuia jeneza lisifukiwe kwa mchanga, wakitaka kufukia jeneza kwa mapesa na walianza kumwaga pesa ndani ya kaburi mpaka pale walipozuiwa.