Kikwete amtembelea Kardinali Pengo Dubai

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amemtembelea Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, nchini Dubai leo.

Kikwete ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter leo(Ijumaa) na kueleza kuwa amemkuta Kardinali Pengo akiwa mwenye siha njema.

Ingawa hajaeleza amemkuta Kardinali Pengo nyumbani au Hospitali lakini askofu huyo mkuu wa jimbo la Dar es Salaam, amewahi kuripotiwa kuwa yupo nje ya nchi kwa matibabu.
View image on TwitterView image on Twitter
Nikiwa Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema.
“Nikiwa Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema.” Ameandika Kikwete

Kikwete amesema amemtembelea Kardinali Pengo wakati akiwa safarini kuelekea Canada.