MAPYA : Zari Atuhumiwa ‘KUFICHA’ Wosia wa Ivan Don, Ndugu Wamuweka Kitimoto #Tazama

Toka Ivan afariki kumekuwa na vuta nkuvute kati ya Zari na ndugu wa Ivan. Zari akihojiwa na Mtandao wa Millard ayo hapo jana alisema kuwa mali za Ivan ana haki ya kuzimiliki yeye kwani walizichuma wote, akiongeza kusema kuwa alioana na Ivan wakiwa hawana Mali hizo, hivyo utajiri wa Ivan una mchango wake mkubwa sana.
Taarifa zilizotufikia Tzee Wire leo hii pia ni kwamba mpaka sasa wosia wa Ivan kuhusu mali zake umepotea na hauonekani, na ndugu wa Ivan wameonyesha wasiwasi wao kuhusu huo wosia na kusema kuwa umefichwa makusudi na Zari ili aubadilishe achukue mali zote yeye. Kutokana na hilo, familia ya Ivan ikiongozwa na baba yake mdogo Ivan,
Umeitisha kikao cha familia na kumtaka Zari ahudhurie akatoe maelezo kuhusu wosia Ulipo. Una Maoni gani Kuhusu hili? Weka maoni yako hapa!!