MPYAA: Picha za Beckham Akiwa Mbugani Zawatoa Mapovu Wasanii wa Bongo..Lulu Amvaa Kichwakichwa Bila Kujielewa #Tazama

David Beckham anaonekana kuwachanganya baadhi ya watu kwa kitendo chake cha kupost picha mitandaoni bila kutaja kama yupo katika moja ya mbuga hapa nchini Tanzania.
Beckham alitua nchini kimya kimya wikiendi iliyopita majira ya usiku akiwa ameongozana na familia yake na kuelekea mahali pasipo julikana huku baadhi ya wadau wakidai alikuwa ameelekea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro.
Kitendo hiko kimewafanya watu kumshambulia kwenye kila picha aliyopost mchezaji huyo wa zamani wa Uingereza.
Hata baadhi ya mastaa wa Bongo wameonekana kushangazwa na kitendo hicho huku wengine wakitoa yao ya moyoni kupitia mtandao wa Twitter, kati yao ni Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Mwasiti. “Mbona hatoi Taarifa kwa wenye nchi Yetu不不不不atajuta nipe username yake kwanza 不不不不hata simfologi,” ameandika Lulu.
Naye Mwasiti ameandika, “ huyu beckham huyu..sasa sisi ni mwendo wa kuweka bendera yetu 屢屢 tu kwenye kila picha yake mbugani kagoma kusema alipo @OfficialLizyM.”
Hata hivyo Fid Q amewachana watu wanaolalamikia tukio hilo, “Nimekuta watu wananung’unika juu ya suala zima la ujio wa DEVI mbugani kwetu eti kwasababu kila akipost hasemi kama yupo TZ..Mlimfadhili? .”