Saida Karoli Awasema Wasanii wa Kike Kupitia ‘Bongo Bahati Mbaya’

Saida Karoli
Msanii wa nyimbo za asili, Saida Karoli amesema kipindi amekaa nje muziki alikuwa akishangaa kuona hakuna msanii wa kike akiimba muziki wa asili zaidi ya kuiga muziki kutoka Ulaya.Akizungumza na kipindi cha Twenzetu cha Times FM, Saida amesema wasanii hao ni sawa na wimbo wa Rapper Young Dee ‘Bongo Bahati Mbaya’ kwa kufanya kila kitu ni Ulaya na si hapa nchini.

“Tatizo nilikuwa sioni wasanii wakiimba nyimbo za asili hasa wanawake, siwaoni. Nawaona wanaimba nyimbo zinazofanana na za Ulaya, mavazi ya Ulaya, sauti ya Ulaya, sioni sauti za Tanzania kwa wanawake,” amesema Saida Karoli.

“Huwezi kutoa maoni kule nilipokuwa, nikasema labda watu wameamua kuwa Ulaya, ndio maana juzi niliongelea wimbo wa tupo Bongo Bahati Mbaya, kila kitu Ulaya, sauti na mavazi yao ni Ulaya,” ameongeza.

By Peter Akaro