Nimeviona Vya Diamond Kuliko Mwanamke Yoyote Adai Hamisa

Nimeviona Vya Diamond Kuliko Mwanamke Yoyote Adai HamisaMzazi mwenza wa Diamond, Hamisa Mobetto alifanikiwa kufanya sherehe ya mtoto wake mwishoni mwa wiki hii na alikuwa na mengi ya kuongea kuhusu mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea mtandaoni.
Maneno mengi yamesemwa juu ya uhusiano wa Diamond, Zari na Hamisa na kwa mara ya kwanza Hamisa ameongea.Hamisa aliweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na Diamond na kuongelea kesi aliyomfungulia mahakamani:Watu inabidi waelewe kitu kimoja, mwanamke hawezi akainuka straight akaenda mahakamani kabla hajaenda mahakamani kuna hatua anatakiwa achukue, unajua mpaka mwanamke aamue kuzaa na mwanaume  ni mpaka mjadiliane na mkubaliane mlee mimba kwa miezi tisa hawezi kurupuka tu akakupeleka mahakani unless huyo mtu hajawahi kupenda, Diamond nimekuwa nae kwenye mahusiano naye kwa takribani miaka tisa siwezi nikaamka tu asubuhi nikakurupuka na kumpeleka mahakamani nakumfungulia mashtaka, kwa sababu hakuna jipya coz kama vitu vya Naseeb hakuna mtu aliyeviona Kama Mimi yaani hakuna mwanamke anamjua vizuri kama mimi ninavyomjua kwa miaka tisa. Kuhusu kufungua kesi yeye ndio aliniambia nitafute mwanasheria ili tutafute njia ya kumhudumia mtoto bila tatizo lolote na lilikuwa wazo lake na sitapendelea kulizungumzia sana hili suala kwa sababu kesi ipo mahakamani”.
Pia Hamisa aliongelea uhusiano wake na Zari na kudai kuwa Hana tatizo lolote na Zari na kusema kuwa hamchukii Zari na ni matumaini take ipo siku wataelewana na kuwa familia kwani watoto wao ni ndugu na hicho ndo cha muhimu.