Ajibu Atoa Shukrani Yanga Awagawa Milioni Moja kwa Wachezaji Wenzake

Ajibu Atoa Shukrani Yanga Awagawa Milioni Moja kwa  Wachezaji Wenzake MSHAMBULIAJI wa Yanga, Ibrahim Ajibu ambaye ni tegemeo hivi sasa jana aliwagawia wachezaji wenzake shilingi 400, 000 kama sehemu ya shukrani kwao baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mbili za Ligi Kuu Bara na kuzawadiwa shilingi milioni moja.
Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu akabidhiwe shilingi milioni moja na Kundi la la Whatsap la Yanga For Life linaoundwa na baadhi ya wasanii ya filamu nchini.
Ajibu alipewa shilingi milioni moja baada ya kufanikiwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu Bara ambazo amezicheza.
Mechi hizo, alizozicheza ni dhidi ya Kagera Sugar ambayo alifunga na kumtengenezea bao moja Mzambia, Obrey Chirwa mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Ajibu aligawa fedha hizo, jana mara baada ya mazoezi ya timu hiyo kumalizika yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kabla ya leo saa 11:30 alfajili kuelekea Mkoani Singida kuvaana na Singida Unite mchezo utakaopigwa keshokutwa Jumamosi Uwanja wa Namfua.
Na Mwandishi Wetu

No comments: