BWANA ARUSI APIGWA RISASI SEHEMU ZA SIRIBwana harusi mmoja chini Misri amepatwa na bahati mbaya ya ajali siku moja kabla ya harusi yake.

Wakati sherehe ilikuwa ikifanyika siku moja kabla ya harusi yake, risasi zilizofyatuliwa kusherekea zilimpiga mguuni, mkononi na sehemu ya nyeti ya uume wake.
Polis waliwaambia waandishi wa habari kuwa bwana harusi alipelekwa hospitalini huku uchunguzi ukiendea.

Mwanamume aliyetajwa kufyatua risasi hizo anaripotiwa kutoroka, lakini baaadaye alikamatwa na polisi.

Kisa hicho kimezua shutuma kwenye mitandao huku watu wengi wakitaka tamaduni ya kufyatua risasi wakati wa sherehe kukomeshwa.

Chanzo: BBC Swahili.

No comments: