IRENE UWOYA NA DOGO JANJA MAMBO YAZIDI KUFICHUKA,CHECK PICHA YAO NYINGINE ILIYOVUJA

HABARI zilizoenea katika mitandao ya kijamii ni kwamba msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Dogo Janja, amefunga ndoa kimyakimya na mnyange wa filamu, Irene Uwoya.
Baada kuenea kwa uvumi huo,  ulifuatilia kujua ukweli juu ya ndoa hiyo iliyowashitua wengi.
Hatua ya kwanza jana ni pale mwandishi wa mtandao alipowaendea wahariri wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers yanayohusiana na habari za wasanii wa Bongo Muvi, Bongo Fleva na wengineo ambapo walijibu kwamba walikuwa wamemtafuta msanii Hamad Aly ‘Madee’ aliyewajibu kwamba alikuwa hajui chochote kuhusu suala hilo.
Mambo hayakuishia hapo kwani wahariri haohao walipowasiliana na Dogo Janja alijibu kwamba na yeye hakujua kinachoendelea.
Mwishoni wahariri wakamalizia kwa kuongea kwenye simu na Irene Uwoya ambapo alipopokea aliulizwa kuhusu suala hilo la kufunga ndoa na Dogo Janja. Jibu la kwanza la mrembo huyo lilikuwa ni: “Mimi ni wa kuolewa? Na nitaolewa na nani? Na iweje niolewe na nyie Global msijue?”
Baada ya kuyasema hayo, muigizaji huyo mahiri wa filamu alimalizia kwa kusema kwamba yote hayo yalikuwa ni muvi ambayo alisema itatokea hivi karibuni.
Leo, Jumapili, mwandishi wa mtandao wetu aliwatafuta tena Madee, Dogo Janja na Irene Uwoya ili kujua iwapo walikuwa wanaendelea na msimamo wao kama walivyowaambia wahariri wetu.
Mambo yalianzia kwa Madee aliyesema ni kweli Dogo Janja amefunga ndoa ila hakutaja alikuwa amefunga ndoa na nani. Mwanamuziki huyo aliye na makazi yake Manzese jijini, alimalizia kwa kuupa mtandao huu namba za simu za Dogo Janja ili uongee naye.
Kilichofuatia ni mtandao kumpigia simu Dogo Janja aliyeipokea na kubadilishana salam na mtandao huu lakini ghafla alinyang’anywa simu na Uwoya aliyesema kwamba ni kweli ‘bwana mdogo’ huyo alikuwa ameoa.
Hata hivyo, hakutaja kama ni yeye aliyekuwa ameolewa, lakini aliongeza kwamba: “Tafadhali tuacheni msitusumbue!”
Mpaka tunakwenda mtamboni, maelezo ya wahusika wote yalikuwa hayajaonyesha moja kwa moja kwamba ndoa hiyo kweli ilikuwa imefungwa baina ya wawili waliotajwa

No comments: