Lazaro Nyalandu Afunguka Kuhusu Kuwepo Kwenye Group La Whatsapp La CHADEMA Nakupanga Na Kupanga...Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa hajawahi kuwa katika kundi la namna hiyo na ni taarifa za uongo zilizotengenezwa kwa lengo la kumchafua.

Nyalandu kupitia mitandao yake ya kijamii ya Twitter, facebook na instagram aliambatanisha picha (screenshot) na kuandika kuwa taarifa inayoonekana ni ya uwongo na ya kufikirika na kuziita siasa za kizamani.

“Fake news alert! Habari hii ni ya kutungwa, kizushi, na kufikirika. Kibaya zaidi, ni ya UONGO. Siasa za aina hii ni za kizamani. Aibu tupu!” ameandika Nyalandu katika mtandao wa Twitter.

Nyalandu ambaye alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge, nyadhifa mbalimbali za uongozi pamoja na uanachama katika Chama cha Mapinduzi na kuomba kuhamia CHADEMA, amepongezwa na baadhi ya viongozi wa upinzani huku baadhi ya viongozi wa chama alichotoka wakimponda.

No comments: