Shamsa Ford Awapa Makavu Wanaomponda Kuuza Duka Badala ya Kumuajili Binti

Shamsa Ford Awapa Makavu Wanaomponda Kuuza Duka Badala ya Kumuajili Binti
MREMBO wa Bongo 
Movies, Shamsa Ford ametoa povu la aina yake kwa mashabiki wanaomponda kwa kitendo cha yeye kuuza duka mwenyewe badala ya kumuweka binti amuuzie.
Akizungumza na Amani, Shamsa ambaye anamiliki duka la nguo na mumewe Chid Mapenzi lililopo Kinondoni jijini Dar, alisema haoni aibu yoyote kuuza mwenyewe dukani hapo kwa sababu ustaa bila kipato chochote ni sawa na mzigo tu hivyo wanaomponda kwenye mitandao ya kijamii wanajisumbua.

“Unajua kuna watu nawashangaa sana wananiambia si nitafute mtu akae dukani halafu mimi nifanye nini? Mastaa wengi wamezoea kulala tu sasa mimi siwezi unapopata fursa ni lazima uitumie ipasavyo,” alisema Shamsa. 

No comments: