Shilawadu Mnaelekea Kaburini Kuna la Kujifunza Toka Kikundi cha ze Comedy ya Masanja

Miaka ya zamani kidogo Kikundi cha ZE COMEDY cha kina Masanja -mkandamizaji na wenzake kilikuwa na umaarufu na hata kupita baadhi wasanii wa muziki wa dansi, bongo fleva na hata bongo movies. Walikuwa wakipata mialiko mikubwa ya pesa ndefu kwenye sherehe, mikutano na majeshini kwenda kutumbuiza watu.


Kuna Kipindi Masanja alikuwa maarufu mpaka alikuwa hawezi kutembea mitaani hovyo bila ya walinzi na alijaribu hata kugombea ubunge katika jimbo moja huko nyanda za juu.Umaarufu wa ZE COMEDY ulianza kupungua baada ya kuanza kufanya vichekesho vya upande mmoja, kufurahisha wakubwa, kulewa sifa na kujiingiza kwenye siasa au kukubali kutumiwa na wanasiasa.

KIPINDI CHAO CHA SAA MOJA USIKU ENZI HIZO KILIKUWA MAARUFU KULIKO HATA TAARIFA YA HABARI.

Kipindi cha SHILAWADU ingawa nao walianza kwa kasi lakini naona wanaanza kuelekea kaburini.Kama SHILAWADU ni kuhusu umbea ni kwanini umbea mwingine wanaogopa kusema ,kwaninini siku hizi kila umbea wanaosema wa msanii unafuatana na kutambulisha wimbo mpya wa msanii, ina maana sio umbeya tena ni vitu mnapanga kabla, matangazo yamekuwa mengi na mmebakiwa na vitu viwili tu ni HAMISA MOBETO na DIAMOND.

Hata leo najua MAPOVU NI HAYO TU na mtakuwa mnaandaa msanii wa kutambulisha ngoma mpya baada ya kutunga skendo, hivi ile ya zamaradi na Ruge mbona ahtukusikia mapovu!!!

KUWENI MAKINI mnaelekea kubaya

By Kasulamkombe

No comments: