Tibaijuka Atangaza Kung'atuka Nafasi ya Ubunge

Tibaijuka Atangaza Kung'atuka Nafasi ya Ubunge
Mbunge wa Muleba Kusini kupitia CCM, Prof. Anna Tibaijuka, ametangaza kung’atuka nafasi ya ubunge kwa kutogombea tena kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Mheshimiwa Tibaijuka alitangaza uamuzi huo walipokuwa wakizungumzia miaka miwili ya Rais John Pombe Magufuli tangu aingie madarakani ambaye alikuwa kwenye ziara mkoani Kagera.
Mama Tibaijuka amekuwa mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 2010, na alishawahi kukumbwa na kashfa kubwa ya pesa za Escrow.
Hivi karibuni Mbunge wa SIngida Kaskazini Lazaro Nyalandu pia ametangaja kujiuzulu ubunge wake na kuomba kujiunga na chama cha CHADEMA.

No comments: